Beki Yanga Ataja Kitakachoiponza Simba SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Beki Yanga Ataja Kitakachoiponza Simba SC-Michezoni leo

BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, amefichua kuwa kwa upande wao, hawana wasiwasi wa kuwafunga Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii, kutokana na wapinzani wao kujiamini sana huku akiamini bado mchezo huo utakuwa mgumu.

 

Yanga na Simba zinatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa kesho Jumamosi huku ikiwa ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ninja alisema kuwa wana nafasi kubwa ya kuwafunga wapinzani wao katika mchezo huo kwa kuwa wamekuwa wakijiamini kupita kiasi tofauti na wao (Yanga).

 

“Kwanza hii mechi itakuwa ngumu kwa timu zote yaani kama haina mwenyewe lakini linapokuja suala la matokeo naona tuna nafasi kubwa ya kuweza kupata ushindi kwa sababu wenzetu wamekuwa wakijiamini sana, kitu ambacho ndiyo kitawaponza.

 

“Unajua wao wamekuwa wakijiamini kupita kiasi kutokana na makombe ya msimu uliopita lakini kwetu tunachoamini nidhamu yetu ndiyo itakuwa kitu bora zaidi kutupa matokeo kwa sababu tutatumia madhaifu (udhaifu) yao ya kujiamini sana,” alisema Ninja.

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Beki Yanga Ataja Kitakachoiponza Simba SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz