Bao la Ronaldo Lamliza Mama Yake-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bao la Ronaldo Lamliza Mama Yake-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Manchester United alimliza mama yake baada ya kufunga mabao mawili.

 

Ronaldo alirejea Uwanja wa Old Trafford akitokea Juventus ikiwa ni baada ya miaka 12 kuyeyuka tangu aliposepa ndani ya timu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer.

 

Mchezo wake wa kwanza Septemba 11 ilikuwa ni wa Ligi Kuu England na alitupia mabao mawili wakati timu yake ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United na mabao yale mengine yalifungwa na Jesse Lingard na Bruno Fernandes kwa upande wa Manchester United.

 

Baada ya kutupia mabao hayo mawili mamayake aitwaye Dolores Aveiro mwenye miaka 66 alishindwa kujiuzia baada ya kushangilia huku akitoa machozi ndani ya Uwanja wa Old Trafford.Inaelezwa kuwa Ronaldo alikuwa hafahamu kuwa mama yake atakuwa hapo kwa sababu alishakatazwa kutazama mechi wakati mwanaye akiwa anacheza.

 

Kazi nyingine kwa Manchester United ni kesho Septemba 14 katika mchezo wa UEFA Champions itakuwa ni dhidi ya Young Boys.

The post Bao la Ronaldo Lamliza Mama Yake appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz