Bado Kuna Kazi ya Kufanya kwa Messi, Ronaldo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bado Kuna Kazi ya Kufanya kwa Messi, Ronaldo-Michezoni leo

MASTAA wawili wakubwa Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo wamekuwa wakitikisa soka la dunia kutokana na ubora wao uwanjani.

 

Dunia nzima imekuwa ikitambua ubora wa mastaa hao kuanzia wanacheza pamoja kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga mmoja akiwa na Barcelona na mwingine akiwa na Real Madrid.

 

Hawa ni mastaa wakubwa sana duniani, hakuna ambao wameweza kucheza kama hawa kwa kipindi chao chote.

Ronaldo kwa sasa anaitumikia Man United ambayo amejiunga nayo hivi karibuni huku Messi yeye akiwa anaitumikia PSG ambayo naye amejiunga nayo hivi karibuni.

 

Wakiwa Hispania mastaa hawa walifanya kila jambo zuri na kuweka rekodi zote kubwa, lakini dunia inasema kuwa kuna rekodi ambazo hawakufanikiwa kuziweka kwa kipindi chao chote wakiwa wanacheza na sasa wanatakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kubwa sana kuhakikisha kuwa wanaziweka.

 

Ronaldo amefanikiwa kutwaa makombe kwenye timu zote ambazo amekwenda, Man United, Sporting Lisbon, Juventus na hata Real Madrid.

Lakini Messi naye ametikisa sana akiwa na timu yake ya Barcelona ambayo amekuwa nayo kuanzia akiwa mdogo sana hadi leo.

 

RONALDO NA MESSI WAMEVUNA NINI HADI SASA

Wamefanikiwa kutwaa makombe mengine yote makubwa, kwenye ngazi ya klabu pamoja na michuano ya kimataifa.

Taarifa inaonyesha kuwa mastaa hao wamefanikiwa kutwaa kila kombe ambalo wamekuwa wakiliwania kwenye kwenye ngazi ya klabu.

 

Ronaldo wiki iliyopita alifanikiwa kuwa kinara wa mabao ya kimataifa duniani ikiwa ni rekodi ambayo ameiwania kwa muda mrefu sana.

Ronaldo akiwa na timu yake ya Ureno alifanikiwa kufunga bao lake la 111 na kuwa kinara wa dunia nzima.

 

Messi, yeye anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora zaidi kwenye La Liga akiwa amefunga mabao 474, lakini akiwa na mabao 120 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Lakini pia Ronaldo naye ameweka rekodi ya kuwa kinara wa ufungaji kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye klabu zote ambazo amefanikiwa kuzichezea akiwa na mabao 134 kwenye timu za Man United Real Madrid na Juventus.

 

Messi pia anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi kwenye La Liga msimu mmoja akiwa amefuga mabao 50, lakini akiwa ametwaa tuzo ya unfungaji bora wa ligi hiyo mara nyingi kuliko mwingine yoyote yule akiwa ametwaa mara nane.

 

RONALDO NA MESSI BADO HAWAJAPATA NINI

Ronaldo pamoja na kwamba yeye ni mfungaji zaidi kwa kipindi chote Ulaya, Messi bado anatakiwa kufunga mabao mawili ili aweke kufikia rekodi ya kuwa mfungaji bora zaidi kwenye ukanda wa Bara la Amerika Kusini.

Messi akifunga mabao mawili ndiyo atakuwa amefikia rekodi ambayo iliwekwa na Pele miaka kadhaa iliyopita.

 

Ronaldo pia anatakiwa kucheza michezo miwili ili afikie rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ili avunje rekodi ya Iker Casillas, aliyecheza michezo 177. Messi yeye amecheza michezo 149.

 

Messi tayari amefanikiwa kutwaa tuzo sita za Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Ronaldo akiwa nazo tano, lakini pia Ronaldo ametwaa makombe matano na Messi manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Mabao je

Kwenye upande wa mabao ya kufunga Ronaldo kwenye klabu zote amefanikiwa kufunga mabao 674, akiwa amemzidi Messi kwa mabao mawili.

 

PARIS, Ufaransa

The post Bado Kuna Kazi ya Kufanya kwa Messi, Ronaldo appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz