Azam Waipigia Mahesabu Mazito Coastal Union-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Azam Waipigia Mahesabu Mazito Coastal Union-Michezoni leo

UONGOZI wa Azam FC umetamba kwamba hauna wasiwasi na wapinzani wao Coastal Union kwa kuwa wamewasoma mapema kabla ya kukutana nao kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 

Azam watakuwa wageni wa Coastal Union katika mchezo huo ambao utapigwa Septemba 27, mwaka huu huku kikosi hicho kikitarajia kusepa leo Jumamosi.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Timu inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa kwanza ambao tutacheza dhidi ya Coastal. Tunatarajia kuondoka kesho (leo) kuelekea Tanga, kocha anasema hana presha kuelekea mchezo huo kwani alishawasoma mapema wapinzani na mazingira ya uwanja anayajua vizuri hata mchezo wa kwanza aliosimamia ulikuwa dhidi ya Coastal kwa hiyo hatuna presha.

 

“Kwenye kikosi chetu hatuna majeruhi zaidi ya Prince Dube ambaye alifanyiwa upasuaji, wachezaji wengine wote wapo fiti na idadi ya wachezaji watakaosafiri itatolewa leo (jana) jioni baada ya mazoezi,” alisema Zaka.

 

Kwe nye kikosi chetu hatuna majeruhi zaidi ya Prince Dube ambaye alifanyiwa upasuaji, wachezaji wengine wote wapo fiti na idadi ya wachezaji watakaosafiri itatolewa leo (jana) jioni baada ya mazoezi,”

 

LEEN ESSAU, Dar es Salaam

The post Azam Waipigia Mahesabu Mazito Coastal Union appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz