Azam Fc Kumkosa Dube Leo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Azam Fc Kumkosa Dube Leo-Michezoni leo

WAWAKILISHI wengine wa Tanzania katika Kombe la shirikisho barani Afrika, Azam FC, leo, Jumamosi watakuwa kwenye dimba  lao la kujidai la Azam Complex jijini Dar es salaam kumenyana na Horseed FC kutoka Somalia katika mechi ya awali ya kombe hilo.

 

Azam ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Horseed FC ambapo itamkosa mshambuliaji wake hatari, Prince Dube ambaye ni majeruhi.

 

Nyota huyo kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini ambapo amefanyiwa upasuaji, uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa maendeleo ya nyota huyo kwa sasa yanaendelea vizuri.

 

Dube ambaye msimu uliopita alitupia mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita.

The post Azam Fc Kumkosa Dube Leo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz