Aucho, Djuma Wakabidhiwa Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Aucho, Djuma Wakabidhiwa Simba-Michezoni leo

WAKIACHWA nchini kiungo Khalid Aucho, Shaban Djuma na Fiston Mayele wameachiwa program maalum mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Septemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mastaa hao wapya wa Yanga wameachwa katika msafara uliosafiri kwenda nchini Nigeria kuvaana dhidi ya Rivers United kutokana na ITC zao kuchelewa kufika.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela alisema kuwa wachezaji hao wanatarajiwa kuwepo kwenye sehemu ya kikosi chao kitakachocheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

“Aucho, Mayele na Djuma wameachwa na kocha Nabi kutokana na ITC zao kuchelewa, hivyo kocha amewaachia program maalum ya mazoezi ya siku tatu.

“Program hiyo wameachiwa kutokana na kuwepo katika mipango ya kocha kwa ajili ya kuwatumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

“Hivyo ni lazima wajiweke sawa ili waendane na kasi ya wachezaji wenzao ambao watacheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Rivers,”alisema Mwakalebela.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Aucho, Djuma Wakabidhiwa Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz