Yanga Yaondoshwa Kagame Cup-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yaondoshwa Kagame Cup-Michezoni leo

YANGA imeondoshwa kwenye michuano ya Kagame Cup baada ya jana kufungwa mabao 3-1 na Express katika mchezo wa mwisho wa Kundi A kwenye michuano hiyo.


Kuondoshwa kwa Yanga
kunatokana na kushika nafasi ya tatu katika kundi hilo baada ya kukusanya pointi mbili zilizotokana na kucheza mechi tatu ambapo sare mbili na kupoteza moja.

Express ndiyo vinara waliokusanya pointi 7, huku Nyasa Big Bullets ikiwa nazo tano na Atlabara mbili.Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, mabao ya Express yalifungwa na Godfrey Lwesibaya dakika ya 15, Muzamiru Mutyaba (dk 37) na Erick Kenzo (dk 53). Bao la Yanga lilifungwa na Paul Godfrey dakika ya 71.

Mchezo mwingine wa kundi hilo uliochezwa jana Uwanja wa Azam Complex, Dar, ulishuhudiwa Nyasa Big Bullets ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Atlabara.

Nyasa Big Bullets na Express zimefuzu nusu fainali ya michuano hiyo sambamba na Azam FC kutoka Kundi B ambapo timu ya nne kutinga hatua hiyo, ilisubiriwa ipatikane kwenye mechi za jana za Kundi B zilizochezwa saa 1:00 usiku.

STORI: LEEN ESSAU, DAR

The post Yanga Yaondoshwa Kagame Cup appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz