Yanga Yafungwa Mabao 2-1 Dhidi ya Zanaco ya Zambia-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yafungwa Mabao 2-1 Dhidi ya Zanaco ya Zambia-Michezoni leo

KIKOSI cha Yanga leo kimepoteza katika mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa.

Alianza  Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 lilikuja kusawazishwa kipindi cha pili Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.

Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.

Mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi na licha ya timu yao kupoteza bado waliwashangilia wachezaji wao.

The post Yanga Yafungwa Mabao 2-1 Dhidi ya Zanaco ya Zambia appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz