PSG Yataja Bei Ya Mbappe Kwa Madrid-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

PSG Yataja Bei Ya Mbappe Kwa Madrid-Michezoni leo

KLABU ya Paris Saint Germain imedai kiasi cha pauni 188m kwa Real Madrid ilikuweza kukamilisha usajili wa Kylian Mbappe imeelezwa.


Juzi ilielezwa kuwa Madrid
waliandaa kiasi cha pauni 137m kwa ajili ya kukamilisha dili la Mbappe kutua kikosini hapo na PSG inaelezwa wamekataa kiasi hicho.

 

Mbappe tayari alieleza kuwa anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho cha PSG ndiyo maana amekataa kuongeza mkataba mpya.

 

Ripoti kutoka Ufaransa zinaeleza kuwa kuwa PSG wao wataka kupokea kiasi cha pauni 188m ili kumuachia staa huyo kikosini hapo.Mkurugenzi wa Soka wa PSG, Leonardo amesema: “Mbappe anataka kuondoka na hilo linaoneka wazi. Kama Madrid wameleta ofa ni wazi anataka kuondoka.

 

“Hatuwezi kubadili mipango yetu katika wiki ya mwisho kabisa ya usajili. Kama anataka kuondoka hatutamkatalia, ila sisi ndiyo tutaweka mezani kitu gani tunahitaji na mfahamu kuwa bado Monaco wanatudai.

The post PSG Yataja Bei Ya Mbappe Kwa Madrid appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz