Pluijm Afunguka Kuwapeleka Yanga FIFA-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pluijm Afunguka Kuwapeleka Yanga FIFA-Michezoni leo

ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amethibitisha kuwa kuna uwezekano mkubwa akaifungulia mashitaka klabu ya Yanga kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘FIFA’ kuhusiana na madai ya stahiki zake.

 

Inaelezwa kuwa kocha huyo anawadai Yanga kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 115 za Kitanzania.

 

Pluijm, aliiongoza Yanga kama kocha mkuu kwa vipindi viwili tofauti kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, huku pia akiwahi kushika nyazifa nyingine ndani ya klabu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema: “Taarifa za mimi kuwa kwenye mpango wa kuwapeleka Yanga FIFA ni za kweli, lakini nisingependa kuzungumza sana kuhusu suala la kesi hii kwa sasa, kwa kuwa kuna wawakilishi wangu ambao wako Dar es Salaam kwa sasa wanashughulikia kesi hii.

 

Gazeti hili pia lilifanya jitihada za kuutafuta uongozi wa Yanga, na kufanikiwa kumpata Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli ambaye alisema: “Taarifa za kudaiwa na kocha Hans zinapaswa kuwekwa sawa kwa kuwa ni kweli alikuwa akitudai lakini tayari suala hili lilishafanyiwa kazi.”

STORI: JOEL THOMAS, CHAMPIONI

The post Pluijm Afunguka Kuwapeleka Yanga FIFA appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz