Mwakinyo: Babu Tale Asinichukulie Poa, Sipigani na Wabeba Matofali – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwakinyo: Babu Tale Asinichukulie Poa, Sipigani na Wabeba Matofali – Video-Michezoni leo

BONDIA namba moja Tanzania na Afrika ambaye pia ni namba 24 Duniani katika uzito wa super welter, Hassan Mwakinyo amesema yeye si mshamba wa magari kama anavyomchukulia Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ ya kutaka kumpiganisha kushindania gari.

 

Mwakinyo (26) ambaye ni bondia mwenye nyota nne amesema ana hadhi kubwa hawezi kupigana na mabondia wadogo wadogo huku akimwahidi kumnunulia magari matatu aina ya Toyota V8 hivi karibuni.

 

“Mimi sio mshamba wa magari kitu ambacho hawakijui, Crown nilimiki mwaka 2016 lakini nilikuwa naogeshea mbwa, namuingiza mbwa kwenye Crown nampeleka baharini akaoge. Nina gari tatu, nina IST, nina gari ndogo ipo hapo nje kwa ajili ya mazoezi tu, kuna gari ya timu halafu kuna Subaru. Ni maisha yangu kwa nini ninyeshe watu, naona kama ni ulimbukeni.

 

“Huwezi kuja kunipiganisha mimi kwa sababu ya gari, huyo Babu Tale mwenyewe ameanza kuendesha magari baada ya kuwa mbunge, zamani alikwa anaendesha magari ya Diamond, chawa wa watu. Kuna vitu mtu anaongea kama kiki, ili watu wamjue.

 

“Familia yangu, baba yangu alikuwa mshua sana, alikuwa tajiri, mimi ndio nimezaliwa nikakuta mambo yameanza kuwa magumu, kwa hiyo wakati natengeneza gym nilikuwa nikichimba chini nakuta mavyuma mazito, maskrepa, hivyo magari yalikuwa sio vitu vya kushangaza. Baba yangu ameendesha magari ambayo watu ndio wanaendesha sasa hivi, mtu anapokuja na mawazo kama hayo unamuona kama hana akili.

 

“Kama wanaweza, bondia yeyote anayetaka kupigana na mimi Tanzania, wamtengeneze afike nyota nne, yani nijue bingwa anapigana na bingwa, sio bingwa anapigana na mbeba matofali, au bingwa anapigana na mbeba mizigo, hiyo ni kashfa, hizo ni dharazu.

 

“Yeye anajua umhimu wa branding ni nini, ndio maana kuna wakati akina Babu Tale hawamuingizi Diamond kwenye vita na wasanii wa chini yake sababu wanaona wanamshusha, kwa nini mimi ananichukulia poa? Sio sawa. I promise nitafika World Champion, na Babu Tale nitamnunulia V8 tatu na sitohitaji chochote kutoka kwake,” amesema Mwakinyo.

The post Mwakinyo: Babu Tale Asinichukulie Poa, Sipigani na Wabeba Matofali – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz