Mukoko Tonombe Kuendelea Kubaki Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mukoko Tonombe Kuendelea Kubaki Yanga-Michezoni leo

UPO uwezekano mkubwa wa kiungo mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu ujao.


Hiyo ikiwa ni siku
chache tangu tetesi zizagae za nyota huyo kutimkia RS Berkane ya nchini Morocco alipokweda kiungo mshambulia wa Yanga, Tuisila Kisinda.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kiungo huyo alikuwepo katika orodha ya wachezaji waliokuwa wanahitajika na Berkane pamoja na Kisinda ambapo kocha wa timu hiyo, Florent Ibenge ndiye anawahitaji.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa bado mazungumzo yanaendelea kati ya Yanga na Berkane kwa ajili ya kufanikisha usajili huo, licha ya kuwepo asilimia chache za nyota huyo kutua hapo.

 

“Kati ya Biashara tuliyokuwa tunaitegemea kuifanya kwa wachezaji wetu, basi Tonombe alikuwepo licha ya Kisinda kutangulia Morocco.

 

Tonombe alitakiwa kuondoka na Kisinda, lakini dili hilo bado halijakamilika na upo uwezekano mkubwa wa kuendelea kuichezea Yanga katika msimu ujao.

 

“Pia yeye mwenyewe Tonombe ameonekana kunogewa kuendelea kuichezea Yanga katika msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, juzi alizungumzia hilo kwa kusema: “Tumepokea ofa za wachezaji wetu kutakiwa na moja ya klabu kubwa, kati ya hao Tonombe ambaye bado dili lake halijakamilka na upo uwezekano mkubwa kubaki Yanga.”

The post Mukoko Tonombe Kuendelea Kubaki Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz