Mshahara wa Banda Simba Kufuru-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mshahara wa Banda Simba Kufuru-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Simba raia wa Malawi, Peter Banda, ameingia kwenye rekodi ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kikosini hapo ambapo kwa mwezi atakuwa akilipwa dola 5000 (zaidi ya Sh 11.6Mil).

 

Banda amejiunga na Simba hivi karibuni akisaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Big Bullets ya Malawi.Vyanzo mbalimbali vinaeleza kwamba, mshahara huo atakaokuwa anaupata Banda amewazidi baadhi ya mastaa kikosini hapo akiwemo John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Joash Onyango, Taddeo Lwanga wanaodaiwa kila mmoja kuchukua Sh 8Mil kwa mwezi.

 

Banda ametua Simba akitajwa kuwa ni mbadala wa Luis Miquissone ambaye dili lake la kujiunga na Al Ahly ya Misri likikaribia kukamilika.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar

The post Mshahara wa Banda Simba Kufuru appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz