Messi Atua Ufaransa, Kusaini Miaka Miwili PSG-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Messi Atua Ufaransa, Kusaini Miaka Miwili PSG-Michezoni leo

ALIYEKUWA staa wa Barcelona, Lionel Messi amekubali kusaini mkataba wa miaka 2️⃣ na PSG ya Ufaransa 🇫🇷 kikiwa na kipengele cha kuongeza hadi Juni 2024.

Messi mwenye umri wa miaka 34 atasafiri leo Jumanne, Agosti 10, 2021, kwenda jijini Paris 🗼 kumaliza dili hilo ambalo atalipwa Paundi milioni 25 kwa mwaka (sawa na Tsh bilioni 80.362) baada ya kukatwa kodi pamoja na bonasi.

Hii imekuja baada ya kuachana na klabu yake ya Barcelona aliyoitumikia kwa miaka 18 kutokana na mkataba wake wa miaka mitano kushindikana kutokana na sheria za La Liga licha ya Messi kukubali kukatwa asilimia 50 ya mshahara wake.

Messi anakwenda kuungana na swahiba wake, Neymar Jr aliyekuwa naye Barca miaka michache iliyopita, Pamoja na Kylian Mbappe na Mu-Argentina mwenzake, Angel Di Maria katika kikosi hicho kinachonolewa na Mauricio Pochettino.

 

The post Messi Atua Ufaransa, Kusaini Miaka Miwili PSG appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz