Messi Aangua Kilio Akiwaaga Barcelona-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Messi Aangua Kilio Akiwaaga Barcelona-Michezoni leo

Wimbo wa mkongwe wa muziki wa Country, Don Williams wa Fare Well Jamaica ndiyo uliomkaa mshambuliaji wa Dunia, Lionel Messi ambaye amejikuta akiangua kilio mbele ya vyombo vya habari wakati akiwaaga mashabiki na viongozi wa Barcelona.

Leo mchana, Messi aliandaliwa mkutano kwenye viunga vya Camp Nou kwenye maskani ya timu hiyo ambapo ameshindwa kabisa kuzuia hisia zake na kujikuta anashindwa aseme maneno gani ya kwaheri Kwa Wana-Barcelona na badala yake akajikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo.

 

Ni ngumu kuamini ila ndiyo hivyo, Barcelona na Messi ambaye ameitumikia klabu hiyo tangu utotoni hadi amekuwa mbaba, wanaachana katika nyakati ngumu sana.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

The post Messi Aangua Kilio Akiwaaga Barcelona appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz