Mbeya City Yaingia Chimbo Kumsaka Mbadala wa Kibu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mbeya City Yaingia Chimbo Kumsaka Mbadala wa Kibu-Michezoni leo

WAKATI ikielezwa kuwa tayari Kibu Dennis amemalizana na Simba kwa ajili ya msimu ujao uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kwamba kwa sasa upo chimbo kusaka wachezaji wapya.

 

Imeelezwa kuwa kwa sasa Kibu yupo Dar kwa lengo la kumalizana na mabingwa wa Tanzania Simba ambao walimpeke ghym kujiweka fiti.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Mathias Rwambiza alisema kuwa hesabu kubwa ni kusajili wachezaji wazuri ili kuziba nafasi kwa ajili ya wale ambao wataondoka.

 

“Ikiwa kuna mchezaji ataondoka basi tutafanya kazi kubwa ya kuweza kumtafuta mbadala wake kwa kuwa hatuwezi kuwazuia wachezaji wetu ambao watahitajika na timu nyingine haitupi tabu.

 

“Wale watakaoondoka basi kazi itakuwa ni kumtafuta mbadala wake kikubwa ni kuona kwamba timu haiypi wala kupoteza ramani,” alisema.

 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Mbeya City Yaingia Chimbo Kumsaka Mbadala wa Kibu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz