Mamilioni ya Mo Yalivyomlainisha Mhilu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mamilioni ya Mo Yalivyomlainisha Mhilu-Michezoni leo

MAPEMA tu, juzi Jumatano, Simba ilimtangaza mzawa, Yusuph Mhilu ambaye ni kiungo mshambuliaji, kuwa mchezaji wao mpya akitokea Kagera Sugar.


Mhilu amesaini dili la miaka
mitatu kuitumikia Simba, huku akidaiwa kukunja zaidi ya shilingi milioni 30 na mshahara mnono kila mwezi.

Chanzo chetu kutoka Simba kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, Simba wamemalizana na Mhilu kabla ya kuzungumza na Kagera Sugar, ambao kimsingi bado wana mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja na mchezaji huyo.

 

Hivyo habari ziko hivi, endapo mabosi wa Simba, watagonga mwamba kupata maridhiano ya usajili wake kutoka kwa Kagera Sugar, ni wazi Mhilu sasa ataneemeka kwa kula mshahara mara mbili kila mwezi.


Championi Ijumaa
limezungumza na Mhilu ambaye amekiri kusaini mkataba wa miaka mitatu simba huku akikiri pia:

“Ni kweli bado nina mkataba na Kagera, ambao kimsingi mimi kama mchezaji haunizuii kusaini Simba, hivyo mimi tayari nimesaini mambo ya mkataba huo watamalizana.

 

“Ujue dili langu kusaini Simba halikuwa na nafasi kubwa ya kuzungumza maana tumekutana siku moja na siku hiyohiyo nikamalizana nao kisha nikasaini, hivyo naamini watamalizana vyema na Kagera ila ikishindikana mimi nipo tayari kurejea Kagera,” alisema Mhilu.

 

Viongozi wa Kagera walipotafutwa jana kulizungumzia hilo simu zao za mkononi ziliita bila kupokelewa lakini Kocha Mkuu wa timu hiyo, Francis Baraza, alisema: “Mimi sijam-release (sijamuachia), maana kocha yeyote anapenda kubaki na mchezaji mzuri. Itabidi waongee wenyewe viongozi kwa viongozi.”

 

Ndani ya Kagera Sugar, Mhilu ambaye alikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ya U-23 kilichotwaa taji la Cecafa Challenge 2021 nchini Ethiopia, alikuwa ni namba moja kwa utupiaji katika misimu miwili mfululizo ambapo ule wa 2019/20 alitupia 13 na ule wa 2020/21 alitupia mabao 9 na kufanya atupie jumla ya mabao 22.

NA STORI NA MUSA MATEJA | CHAMPIONI

The post Mamilioni ya Mo Yalivyomlainisha Mhilu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz