Kocha Yanga Matumaini Kibao Dhidi ya Rivers United-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kocha Yanga Matumaini Kibao Dhidi ya Rivers United-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amefunguka kuwa mpango wake mkubwa ni kuhakikisha wanautumia mchezo wao wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Zanaco FC ya Zambia, kuhakikisha wanafanya vizuri dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

 

Yanga imepangwa kucheza na Rivers United katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika
unaotarajiwa kupigwa kati ya Septemba 10 hadi 12, mwaka huu.


Katika mchezo huo, Yanga wanatarajia kuanzia nyumbani, kabla ya kwenda kumalizia ugenini kati ya Septemba 17 na 19, mwaka huu.


Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusu mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United, Nabi alisema: “Tumerejea Dar es Salaam baada ya kuwa na kambi ya muda kule nchini Morocco iliyokuwa na lengo la kutuandaa na msimu mpya, mbele yetu tuna matukio mawili makubwa ambayo tunajiandaa nayo.


“Kuna mchezo wa Kilele cha Wiki ya Mwananchi tutakaocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia.


“Benchi la ufundi tumejipanga kuutumia mchezo huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi dhidi ya Rivers United yaNigeria.
“Tunawafahamu Zanaco, tunaamini ni kipimo sahihi kwetu kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Stori: JOeL THOMAS, Dar es Salaam

The post Kocha Yanga Matumaini Kibao Dhidi ya Rivers United appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz