Kiungo wa Simba Aibukia KMC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kiungo wa Simba Aibukia KMC-Michezoni leo

JINA la Said Ndemla kwa sasa lipo katika makaratasi ya KMC hiyo ni kutokana na kiungo huyo kuwepo katika mipango ya klabu hiyo ambayo inamuhitaji mchezaji huyo kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima.

 

Ndemla bado ana mkataba wa kuitumikia Simba wa mwaka mmoja kutokana na kiungo huyo kusaini mkataba wa miaka mawili mara baada ya mkataba wake wa awali kumalizika katika msimu wa 2019/2020.

 

Chanzo cha uhakika kutoka KMC kililiambia Championi Jumatano kuwa, wapo katika mipango ya kumsajili Ndemla kwa mkopo hivyo kwa sasa wanafanya mazungumzo na Klabu ya Simba ili kuona kama watampata kiungo huyo.

 

“kwa sasa tupo katika mazungumzo na klabu ya Simba ili tuweze kumpata Ndemla kwa mkopo wa msimu mzima, kila kitu kinaendelea vizuri na kama mambo yatakamilika basi kila kitu kitawekwa hadaharani,” kilisema chanzo hiko.

 

Alipotafutwa Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala azungumzie ishu hiyo alisema: “Kwa sasa tupo katika masula ya msiba wa aliyekuwa mmoja kati ya wafanyakazi wetu wa KMC, hivyo tutazungumza masuala ya usajili pindi tutakapomaliza masuala haya.”MARCO MZUMBE,Dar es Salaam

The post Kiungo wa Simba Aibukia KMC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz