Kane Aitega Spurs-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kane Aitega Spurs-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane imeripotiwa kuwa anataka kulipwa mshahara wa Paundi 400,000 sawa na Bil. 1.2 na ushee hivi za kitanzania kwa wiki, na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu zaidi ligi kuu ya England.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Spurs kumbania Kane kwenda Manchester City kwenye majira haya ya kiangazi, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, Kane aliiandika kuwa atasalia msimu huu katika timu hiyo na atajitolea kwa 100% kuisaidia klabu hiyo.

 

Kevin de Bruyne wa Manchester City ndiye anaoongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu kwenye Epl akipokea paundi 385, 000 na mlinda mlango wa Manchester United David de Gea akilipwa 350,000 kwa wiki, wengine ni Paul Pogba paundi 300,000 na Kane ambaye pia kwa sasa ndani ya Spurs anakunja paundi 300,000.

The post Kane Aitega Spurs appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz