Ibenge Afunguka Dili la Kisinda Kutua Morocco-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ibenge Afunguka Dili la Kisinda Kutua Morocco-Michezoni leo

HATIMAYE Kocha wa RS Berkane ya nchini Morocco, Frolent Ibenge amefunguka juu ya dili la winga wa Yanga, Tuisila Kisinda kujiunga na klabu hiyo ambayo anaifundisha.

 

Ikumbukwe Ibenge ndiye kocha aliyemkuza winga huyo tangu akiwa na umri wa miaka 19 walipokuwa katika kikosi cha AS Vita ya nchini DR Congo.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatano moja kwa moja kutoka nchini Morocco, Ibenge alisema kuwa amezisikia taarifa za winga huyo kuhusishwa kujiunga na timu yake na ni jambo zuri kwa kuwa Kisinda ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa.

 

“Nimesikia kuhusu Berkane kumuhitaji Kisinda, ni mchezaji mzuri ambaye namfahamu tangu hapo awali tukiwa wote AS Vita, sio mbaya sisi kuhusishwa naye, ila kwa sasa siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa bado haijathibitishwa kuwa ni mchezaji wetu,” alisema kocha huyo.

The post Ibenge Afunguka Dili la Kisinda Kutua Morocco appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz