Huyu Ndo Mbadala wa Tusila Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Huyu Ndo Mbadala wa Tusila Yanga-Michezoni leo

TAARIFA kutoka nchini Burkina Faso zinasema kuwa, Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, @yangasc wametua katika Klabu ya Cotonsport FC de Garoua ya Cameroon kumnasa kiungo mshambuliaji wa Timu hiyo, Sibiri Arnaud Sanou (22) kama mbadala wa Tuisila Rosien Kisinda.

 

Sanou ambaye pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Burkina Faso amefunga mabao matatu na assist 2 kwenye mechi 13 za Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup).

 

Awali ililipotiwa kuwa, Klabu ya Yanga SC 🇹🇿 wapo katika mazungumzo ya kumsajili wingi wa klabu ya AS Vita Club 🇨🇩 Jésus Ducapel Moloko 🇨🇩⬅mwenye umri wa miaka (22) kuchukuwa nafasi ya Tuisila Kisinda 🇨🇩 ambae anajiunga na klabu ya ➡ RS Berkane ya Morocco 🇲🇦..

 

Katibu Mkuu wa Yanga Sc Haji Mfikirwa amethibitisha kuwa winga wao Tuisila Kisinda 🇨🇩 anaondoka na sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mbadala wake.

 

The post Huyu Ndo Mbadala wa Tusila Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz