Hukumu Kesi ya Morrison CAS Yasogezwa Mbele-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Hukumu Kesi ya Morrison CAS Yasogezwa Mbele-Michezoni leo

MAHAKAMA ya usuluhisho masuala ya mpira kimataifa ‘CAS’ imesogeza mbele hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji Benard Morrison iliyokuwa isikilizwe Agosti 26,2021.

 

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na CAS ikisainiwa na mshauri wao, Caroline Fischer imeomba radhi kwa pande zote mbili na kusogeza kesi hiyo mpaka Septemba 21,2021.

 

“Kwa niaba ya Rais wa mahakama ya usuluhisho (CAS) tunaomba pande zote mbili zipokee samhani ya kuchelewa kwa kutolewa rasmi maamuzi ya kesi, bado inafanyiwa kazi kwa kutoangalia upande wowote,”imesomeka taarifa hiyo iliyoandikwa na Fischer.

 

Ikumbukwe Yanga walimfungulia kesi Morrison katika kamati ya Hadhi, Sheria za wachezaji kwenye Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na kushindwa kesi hiyo ndipo wakafungua kesi nyingine CAS ambayo sasa hukumu yake itakuwa Septemba 21.

The post Hukumu Kesi ya Morrison CAS Yasogezwa Mbele appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz