Gomes Awapa Majukumu Mazito Sakho, Banda-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Awapa Majukumu Mazito Sakho, Banda-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa, tayari ameanza waelewa wachezaji wapya wa
timu hiyo wakiwemo Peter
Banda na Pape Ousomane Sakho baada ya kuwataka kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao katika kila mchezo.


Sakho raia wa Senegal,
amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Teungueth sawa na Peter Banda raia wa Malawi, aliyejiunga na timu hiyo akitokea Big Bullets ya kwao Malawi.

 

Wachezaji hao kwa sasa wapo na timu hiyo katika kambi ambayo Simba imeweka nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Gomes alisema kuwa amekuwa akivutiwa na uwezo unaonyesha na wachezaji wapya wa timu hiyo wakiwemo Banda na Sakho hali iliyopelekea kuwataka kuongeza juhudi za kutengeneza nafasi za kufunga kabla ya kuanza kwa ligi.

 

“Nadhani tuna timu nzuri kwa sababu wachezaji wetu bado wapo kwenye hali nzuri na wanaonyesha wapo tayari kwa ajili ya kutetea ubingwa wetu wa ligi pamoja na mikakati ya kuhakikisha tunafika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu aina ya wachezaji ambao nipo nao kwa sasa.

 

Kuhusu wageni wote ni wachezaji wenye ubora na viwango vikubwa, imani yangu wataweza kutoa ushindani wa kutosha kwa wachezaji waliowakuta, angalia mtu kama Banda na Sakho hasa kwa nafasi ambazo wanacheza wanakila sababu za kuhakikisha wanatengeneza nafasi zaidi kuanza sasa pamoja na kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,” alisema Gomes.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

 

The post Gomes Awapa Majukumu Mazito Sakho, Banda appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz