DTB Wamepania Ligi Kuu, Tambwe Ndani-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

DTB Wamepania Ligi Kuu, Tambwe Ndani-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC na Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya DTB FC ambayo msimu ujao itacheza Championship.

 

Tambwe alitambulishwa hivi karibuni kuwa mchezaji wa DTB ambapo ataungana na mastaa wengine kama Juma Abdul, David Mwantika na Yannick Bazola ili kukiimarisha kikosi hicho kilichopania kucheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTB FC, Muhibu Kanu, alisema: “Maandalizi mpaka sasa yapo vizuri na tumemsajili Tambwe na nyota wengine, hadi sasa timu tayari ipo kambini ikiendelea na mazoezi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ambao pia tutautumia kama uwanja wetu wa nyumbani kwenye ligi.

 

“Tumekwisha maliza kusajili na mpaka sasa tuna wachezaji 26 ambao kati yao wachezaji sita ni wa kigeni, mpango wetu kwa sasa ni kuhakikisha tunafanikiwa kufika ligi kuu.”Imeandikwa na Onesmo Milanzi (SJMC), Jonas Makore na Richard Ngailla (Tudarco)

The post DTB Wamepania Ligi Kuu, Tambwe Ndani appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz