Djuma Ataja Siku ya Kutua Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Djuma Ataja Siku ya Kutua Yanga-Michezoni leo

WACHEZAJI wapya wa Yanga, Fiston Mayele na Shabani Djuma, wanatarajiwa kutua mapema wiki hii tayari kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 15, mwaka huu.


Nyota hao ambao
msimu uliopita walikuwa wakiitumikia AS Vita ya DR Congo, tayari wameshakamilisha usajili wao wa kuitumikia Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema kabla ya kufika Agosti 13, atakuwa ameshawasili Tanzania akiwa sambamba na Djuma tayari kwa ajili ya kujiunga na kambi ya Yanga.

 

“Wiki hii natarajia kurudi tena Tanzania mara baada ya kusaini mkataba na kuondoka kurejea nyumbani, hivyo nitakuwa huko kabla ya tarehe 13 kwa ajili ya kujiunga rasmi na kambi ya timu itakayoanza Agosti 15.

 

“Natarajia kuja Tanzania nikiongozana na Djuma Shabani na Tuisila Kisinda ambaye sina uhakika sana kama itakuwa hivyo, lakini niliambiwa hivyo na viongozi,” alisema mshambuliaji huyo.

 

Kwa upande wa Djuma, alisema: “Nakuja Tanzania muda sio mrefu, Wanayanga nisubirini ninakuja kufanya kazi, nahitaji sapoti yenu.

STORI NA MARCO MZUMBE NA CAREEN OSCAR Dar

The post Djuma Ataja Siku ya Kutua Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz