Chama: Usajili Yanga Unashtua-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Chama: Usajili Yanga Unashtua-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, amekiri kuwa usajili unaofanywa na wapinzani wao Yanga kwa ajili ya msimu ujao unashtua huku akisisitiza msimu ujao utakuwa mgumu zaidi.


Chama amekwenda mbali zaidi
kwa kuwataja na Azam kuwa pia wamepania kufanya vizuri kwenye msimu ujao kutokana na kushusha wachezaji wa maana kutoka sehemu mbalimbali.

 

Kauli ya kiungo huyo imekuja kufuatia Yanga kutambulisha wachezaji wapya watatu ambao ni washambuliaji, Fiston Mayele kutoka AS Vita ya DR Congo na Harietier Makambo pamoja mshambuliaji mzawa kutoka Biashara United, Yusuph Athuman huku ikielezwa kuwa imeshamalizana na beki wa AS Vita, Djuma Shabaan.

 

Kwa upande wa Azam tayari imeweka wazi usajili wa nyota wapya saba kwa ajili ya msimu ujao ambao ni Ahmed Ali Salim kipa kutoka KMKM, beki wa kushoto, Edward Manyama, viungo, Paul Katema, Charles Zulu na Rogers Kola (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya) na Idris Mbombo raia wa DR Congo.

 

Akizungumza na mshabiki juzi kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Chama alisema kuwa anaamini msimu ujao wa ligi utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wao wanavyofanya usajili wa wachezaji wazuri.

 

“Natamani kuona msimu ujao maana naona utakuwa na ushindani zaidi, nasema hivi kwa sababu naangalia usajili ambao unafanywa kutoka Yanga na Azam pia, Azam wamefanya usajili mzuri sana, naona wataongeza ushindani katika kupambania ubingwa maana wataondoa ile hali ya ligi kuwa Simba na Yanga pekee.

 

Nadhani wakati huu wamefanya usajili mzuri na hata ukiangalia wachezaji wengi waliosajiliwa nawajua, watatengeneza timu nzuri lakini hata Yanga wamefanya usajili mzuri ila kama hawatajipanga itakuwa bure maana Simba umoja ndiyo jambo muhimu hata ukiangalia kauli mbiu ya nguvu moja pamoja na upendo uliopo unatufanya kuwa kitu kimoja wakati wote,” alisema Chama.

STORI NA IBRAHIM MUSSA

The post Chama: Usajili Yanga Unashtua appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz