Breaking: Yanga Yamtangaza Senzo Kuwa Mtendaji Mkuu – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Breaking: Yanga Yamtangaza Senzo Kuwa Mtendaji Mkuu – Video-Michezoni leo

MAKAMU Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela leo Agosti 31, 2021 amemtangaza, Senzo Mbatha kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu hiyo atakayesimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Hajji Mfikirwa atakuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

 

Mwakalebela amesema Kamati Tendaji wanapenda kumpongeza aliyekuwa Kaimu Katibu wa Klabu hiyo, Hajji Mfikirwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya klabu hiyo.

 

Akiongea Kaimu C.E.O mpya, Senzo amewashukuru Kamati Tendaji ya Klabu hiyo kwa kumchagua katika nafasi hiyo na atafanya kazi kwa kushirikiana na timu nzima ya Uongozi, wanachama na mashabiki.

Fredrick Mwakalelebela ametangaza hayo baada ya katiba ya Yanga kubadilishwa baada ya wanachama wa klabu hiyo kupitisha mchakato wa mabadiliko kwa asilimia mia.

The post Breaking: Yanga Yamtangaza Senzo Kuwa Mtendaji Mkuu – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz