Ambundo Atulizapresha Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ambundo Atulizapresha Yanga SC-Michezoni leo

LICHA ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Kagame, kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Dickson Ambundo amewashusha presha Wanayanga kwa kusema anaamini kikosi chao kina nafasi kubwa na kitashinda makombe kwa msimu ujao wa 2021/22.

 

Ambundo amejiunga na Yanga katika dirisha hili la usajili akitokea klabu ya Dodoma Jiji baada ya kuwa na wakati mzuri msimu uliopita, akihusika kwenye mabao 11 msimu uliopita akifunga mabao manne na kuasisti mara saba kwenye michuano yote.

 

Ambundo amefanikiwa kuonyesha kiwango bora tangu ajiunge na Yanga ambapo mpaka sasa amecheza michezo mitatu kwenye michuano ya Kombe la Kagame na kuhusika kwenye bao moja kwa kutoa asisti ya bao la Waziri Junior kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ambundo alisema: “Licha ya kutolewa kwenye michuano ya Kagame, lakini nashukuru Mungu kwa kuanza vizuri kwenye klabu hii, najua nina deni kubwa kwa Wanayanga, kuhakikisha nafanya vizuri na kurejesha furaha yao kwa kushinda makombe.

 

“Haiwezi kuwa kazi rahisi, kutokana na ushindani mkubwa wa namba nitakaokabiliana nao, lakini nipo tayari kwa ajili ya kupambana na changamoto ya mazingira haya mapya na kuendelea kucheza kwa kiwango cha juu ili kuisaidia Yanga kushinda makombe msimu ujao.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Ambundo Atulizapresha Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz