Wachezaji Yanga Waogelea Mamilioni-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wachezaji Yanga Waogelea Mamilioni-Michezoni leo

Mfadhili wa Klabu ya Yanga, Ghalib Salim Mohamed ‘GSM’ ameripotiwa kutoa Shilingi milioni 500 kwa wachezaji wa klabu hiyo, baada ya kuibanjua Simba SC, Jumamosi iliyopita (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

GSM ameripotiwa kutoa zawadi hiyo, kama kutimiza ahadi yake kwa wachezaji wa Young Africans ambao alikutana nao kabla ya kukutana na Simba SC, na kuwaahidi endapo watashinda atawapatia kiasi hicho cha pesa.

 

Taarifa kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo ni kwamba hawakutaka kupishana na fedha hizo na kwamba walitambua viongozi wao wanataka ushindi nao wakafanya kweli.

 

Hesabu za harakaharaka ni kwamba kuna uhakika kila mchezaji haitapungua kiasi cha Shilingi milioni 20 katika ahadi hiyo ya vigogo wa klabu yao.

 

Ahadi hiyo inaweza kuwashtua wengi kutokana kuwa ndio ahadi kubwa kwani hakuna klabu imewahi kutoa ahadi kubwa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara zaidi ya hiyo kwa msimu huu 2020/21.

 

Bao la ushindi la Young Africans katika mchezo wa Jumamosi (Julai 03) lilifungwa na kiungo mzawa Zawadi Mauya dakika ya 11, kwa kupiga shuti kali lililombabatiza beki wa pembeni wa Simba SC, Shomari Kapombe.

 

Ushindi huo umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 70, huku ikisalia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Simba SC ikiwa kileleni kwa kumiliki alama 73.

 

The post Wachezaji Yanga Waogelea Mamilioni appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz