Simba Yashikwa Pabaya na Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Yashikwa Pabaya na Yanga-Michezoni leo

KUELEKEA fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam itakayopigwa Julai 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, kasi ya Yanga imewashitua Simba ambao wamelazimika kupunguza shamrashamra za ubingwa wao ili kupata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo.

 

Leo jioni kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Simba wanatarajiwa kukabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu Bara walilolitwaa msimu huu kwa mara ya nne mfulululizo, baada ya mchezo dhidi ya Namungo.Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusiana na sherehe za ubingwa wao, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Kwa sasa tumewekeza mawazo yetu kwenye mchezo dhidi ya Namungo utakaochezwa kesho (leo) Jumapili.

 

“Utaratibu wa sherehe za ubingwa utatolewa rasmi na uongozi wa juu, lakini hata hivyo hatutarajii kuwa na sherehe kubwa kwa sababu bado tuna mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga na tunataka kuanza mapema maandalizi ya mchezo huo kwa kuwa malengo yetu ni kutetea kombe hilo.”

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kutibua sherehe za ubingwa wa Simba, ambapo msimu uliopita ilitokea hali kama hiyo ambapo timu hiyo ilipokuwa chini ya Kocha Sven Vandenbroeck.

 

Simba ilikabidhiwa ubingwa wao katika mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa mkoani Lindi, ilipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar, kulikuwa na maandalizi ya kusherehekea ubingwa huo kwa kuandaliwa gari la wazi.

 

Sven aligomea sherehe hizo akitaka vijana wake waingie kambini kujiandaa kuwakabili Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam uliochezwa Julai 12, mwaka jana Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

The post Simba Yashikwa Pabaya na Yanga appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz