Nahodha wa Ghana Andre Ayew kujiunga na Al Sadd SC ya Qatar-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nahodha wa Ghana Andre Ayew kujiunga na Al Sadd SC ya Qatar-Michezoni leo

Nahodha wa timu ya soka ya Ghana Andre Andreyeye yuko tayari kusaini makubaliano na klabu ya Qatar Al Sadd SC. Klabu hiyo inasema imefikia makubaliano ya kumsaini nahodha huyo wa Black Stars.

 

Kijana huyo wa miaka 31 anasafiri kwenda Qatar kukamilisha kusaini mkataba.Ayew anatarajiwa huko Doha Alhamisi (leo) kufanyiwa matibabu na baadaye kutia saini makubaliano hayo.

 

Ayew amekuwa hana kilabu baada ya kandarasi yake ya miaka mitatu na klabu ya Wales Swansea City kukosa kuongezwa mwishoni mwa msimu uliopita. Ilikuja wakati klabu ilikosa kupanda hadi Ligi ya Premia dhidi ya Brentford katika fainali ya mchujo.Ripoti zinaonyesha kuwa tapata zaidi ya dola laki mbili ($ 200, 0000) kwa wiki.

 

Uhamaji wake ni sawa na mtangulizi wake kama nahodha wa Ghana Asamoah Gyan ambaye aliacha ligi ya Uingereza na kucheza Mashariki ya Kati wakati alihama kutoka Sunderland kwenda Al Ain huko UAE.

The post Nahodha wa Ghana Andre Ayew kujiunga na Al Sadd SC ya Qatar appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz