Mzee Mpili: Kwani Wao Wanasemaje?-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mzee Mpili: Kwani Wao Wanasemaje?-Michezoni leo

MZEE MPILI ni miongoni mwa wanachama wakongwe wa kablu ya #yangasc. Siku za hivi karibuni Mzee Mpili amejizoelea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Umaarufu wa Mzee Mpili ndani ya Yanga ni kama anachukua nafasi ya marehemu Mzee Akili Mali ila wawili hawa wana utofauti mkubwa katika maongezi na mitazamo yao ndani ya klabu yao pendwa.

 

Maongezi ya Mzee Mpili mara nyingi yamejikitika zaidi katika kamati za kiufundi za nje ya uwanja na hii huwenda ndiyo ikawa tofauti yake na Mzee Akili Mali. Wapenzi wengi wa soka wanamkumbuka zaidi Mzee Akili Mali zama za Uongozi wa Yusuph Manji.

 

Kabla ya mechi ya Watani wa Jadi #derby ya kariakoo mzee huyu kutoka Ikwiriri mara kadhaa alisikika akijinasibu na kujigamba kuwa Mnyama #simbasc hatoki Jumamosi ya Julai.

 

“Mimi ninakuambia sisi tunawapiga wale, wameshakwisha, mimi nina watu,”- Kauli ya Mzee Mpili a.k.a mzee wa Nyuklia siku nne kabla ya kucheza na Mtani Simba.

 

Mechi hiyo ilimalizika kwa Yanga kuifunga Simba bao 1-0, katika Dimba la Mkapa, bao ambalo lilifungwa na kiungo Zawadi Mauya dakika ya 12 tu ya mchezo huo.

The post Mzee Mpili: Kwani Wao Wanasemaje? appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz