Mwakalebela: Tutaifunga Tena Simba Kigoma-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwakalebela: Tutaifunga Tena Simba Kigoma-Michezoni leo

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema baada ya ushindi dhidi ya Simba kwenye mchezo uliopigwa Julai 3, mwaka huu kwenye Dimba la Mkapa, Dar, wapo tayari kwa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, Julai 25, mwaka huu.

 

Jumamosi iliyopita, Yanga iliifunga Simba bao 1-0 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo timu hizo zitakutana katika fainali ya Kombe la Shirikisho, Julai 25 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

 

Mwakalebela alisema: “Mechi ya ligi ilikuwa ni ya kutafuta heshima na tumefanikiwa kuwafunga Simba, hivyo mechi ya Kigoma tunakwenda kufanya kazi na nina imani tutalitwaa Kombe la Shirikisho.

 

Tunajua udhaifu wa Simba ulipo ndiyo maana wamekuwa wakisumbuka kupata matokeo mbele yetu kwa msimu wa pili mfululizo.“Benchi la ufundi, wachezaji pamoja na viongozi tunafanya kazi kwa kushirikiana ndiyo maana tumeweza kulifanikisha hili na Kigoma pia tutakwenda kufanikiwa, kikubwa mashabiki waziidi kutuunga mkono.”

Stori: HUSSEIN MSOLEKA, Dar es Salaam

The post Mwakalebela: Tutaifunga Tena Simba Kigoma appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz