Manara: Naacha Kazi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Manara: Naacha Kazi-Michezoni leo

MSEMAJi wa Klabu ya Simba, Haji Manara kuelekea mechi ya fainali kombe la Azam Shirikisho, Julai 25 mkoani Kigoma dhidi ya Yanga amesema endapo timu hiyo itafungwa tena basi atajiuzulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo.

 

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Manara ameandika; “Unafika Pemba kutokea Airport hadi kinyasini Wete Pemba kote barabarani watu wametinga jezi za Mnyama. Wapemba hawajali kuhusu matokeo ya juzi,,before sikuwa najua Pemba ina Simba wengi kiasi hiki aiseee.

 

“Captain John Bocco sema na wenzio bro, mtakuja kuua watu Kwa makundi siku moja, naambiwa Dar kuna Shabiki kajipiga kitanzi huko, halafu ya kwanza mmecheza kama mmelazimishwa au mnadai kitu, mmezinduka second half na wao wakaweka contena mechi ikaisha.

 

“Wallah Kigoma tukifungwa naacha hii kazi narudi shamba kulima, viongozi wanatimiza majukumu yao, washabiki wanajaa kuliko washabiki wao kwa mbali mno, mimi natukanwa kutwa kwa kuwapa nguvu nyie, lakini mmeenda kutuangusha.

 

“Sioni sababu ya kuendelea na kazi hii kama wachezaji hawajui nini maana ya uzito wa Derby, wachezaji wao wanajitoa asilimia elfu moja toka dakika ya kwanza, sisi tunazinduka kushakuchwa, kaeni wenyewe zungumzeni na thamani ya jezi ya Simba ilindwe….”

The post Manara: Naacha Kazi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz