Kumbe! Manara Anatembea Na Mkataba Wa Milioni 4 -Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kumbe! Manara Anatembea Na Mkataba Wa Milioni 4 -Video-Michezoni leo

HANS Poppe Zakaria, Mwanachama wa Klabu ya Simba amesema kuwa hajapendezwa na tabia ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kusikika akimlalamikia Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

 

Hivi karibuni imekuwa ikisambaa sauti ya Manara ikidai kwamba anachukiwa na Barbara ambaye amekuwa akiwadhalilisha wafanyakazi. Pia ilienda mbali sauti hiyo ikaeleza kuwa Manara anafanya kazi kubwa bila mkataba na analipwa laki 7 kwa mwezi.

 

Sakata hilo limezidi kuwa la moto ambapo Manara kupitia mitandao ya kijamii amesema kuwa baada ya mchezo dhidi ya Yanga kuisha ataongea kwa kuwa sauti ambazo zinasambaa kwa sasa ni za muda mrefu.

 

Hans amesema kuwa kitendo cha Manara sio kizuri hasa kuelekea kwenye mchezo mgumu dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika na amebainisha kuwa alipewa mkataba wa milioni 4 bado hajasaini.

 

“Kitendo ambacho amekifanya Haji sio kizuri na sijakipenda hata kidogo hasa kwa kumfanyia bosi wake. Nipo ndani ya Simba na ninajua kwamba kuna miiko ya kazi lakini kwa Manara amefanya jambo ambalo halipo katika miiko.

 

“Labda anaona kwamba yeye ni mkubwa kuliko Simba hiyo sio sawa lazima amuheshimu bosi wake na kuna utaratibu wa kufanya katika mambo kama haya pale yanapotokea.

 

“Nimeskia analalamika kuhusu mshahara wa laki 7 basi aseme kuhusu mkataba wa milioni 4 ambao amepewa ili asaini, mbona amepewa muda mrefu na hajasaini kwa nini?.

The post Kumbe! Manara Anatembea Na Mkataba Wa Milioni 4 -Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz