KMC Yagoma Kuipa Ubingwa Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

KMC Yagoma Kuipa Ubingwa Simba-Michezoni leo

UONGOZI wa Klabu ya KMC, umefunguka kuwa, timu yao ipo kwenye maandalizi mazuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa kesho Jumatano dhidi ya Simba, na hawaendi kukamilisha ratiba ya kuwapa ubingwa wapinzani wao hao.

 

KMC kesho watakuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Simba ikiibuka na ushindi kwenye mchezo huo, itakuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 76 ambazo Yanga inayoshika nafasi ya pili inaweza kuzifikia ikishinda mechi zake mbili zilizosalia, lakini itazidiwa uwiano wa mabao na kuifanya Simba kuwa bingwa kabla ya kumalizia mechi tatu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, alisema: “Tunaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa Jumatano, ni wazi tunatarajia mchezo mgumu kwa kuwa wapinzani wetu ni timu bora, na wanatoka kupoteza mchezo muhimu wa dabi.

 

“Hivyo malengo yao makubwa yatakuwa kusaka ushindi kwa namna yoyote ile, ili wajipoze na ubingwa, lakini niwaweke wazi kuwa tumekuwa na muda mrefu wa maandalizi ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huu, na hatuwezi kukubali kutoa tiketi ya ubingwa bali tutapambana kufanikisha malengo yetu.”

 

STORI: JOEL THOMAS NA HAWA ABOUBAKHARI

The post KMC Yagoma Kuipa Ubingwa Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz