Kisa corona, Kambi ya Arsenal Marekani Yayeyuka-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kisa corona, Kambi ya Arsenal Marekani Yayeyuka-Michezoni leo

ARSENAL imelazimika kujitoa katika michuano ya Florida Cup ambayo itafanyika nchini Marekani, baada ya baadhi ya watu ambao walitakiwa kwenye msafara wao kupata maambukizi ya Covid-19.

 

Arsenal ilitarajiwa kwenda Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na kushiriki michuano ya Florida Cup.

 

Michuano hiyo, inatarajiwa kuanza Julai 26, mwaka huu na Arsenal mchezo wa kwanza ilipangwa kucheza dhidi ya Inter Milan.

 

Arsenal ilitoa taarifa yake rasmi juu ya kujitoa katika michuano hiyo iliyosema: “Katika kundi letu kuna baadhi wamebainika kuwa na maambukizi, kutokana na hali hiyo tumelazimika kujitoa kwenye mashindano ya Florida Cup.“Haya ni maamuzi magumu lakini hii imetokana na afya za wachezaji pamoja na stafu wetu.

 

Tunajua tumeangusha mashabiki wetu wa Marekani ambao waliamini kuwa wangetuona kipindi hiki cha maandalizi ya msimu mpya.

 

Pia tunaomba samahani kwa waandaaji wa mashindano ya Florida Cup kwani walitumia muda kuandaa michuano hii na wakatualika. Tunaamini mtatuelewa kutokana na kuwa na wakati mgumu kwa sasa.”

The post Kisa corona, Kambi ya Arsenal Marekani Yayeyuka appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz