Gwambina Yavunja Mlango, Yadaiwa Laki Tano-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gwambina Yavunja Mlango, Yadaiwa Laki Tano-Michezoni leo

TIMU ya soka ya Gwambina ya mkoani Mwanza italazimika kulipa shilingi laki tano kutokana na kuvunja geti dogo la Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.

 

Geti hilo walilivunja mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mchezo wao dhidi ya Mbeya City uliyomalizika kwa Mbeya City kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Kibu Denis.

 

Kwenye mchezo huo kulitawaliwa na imani za kishirikina ambazo zilisababisha timu hiyo kutotumia geti rasmi. Meneja wa uwanja huo Modestus Mwaluka amesema gharama za mlango pamoja na matengezo ni laki tano na elfu kumi na mbili (512,000).

 

“Taarifa imefika sehemu husika na gharama zake ni laki tano na elfu kumi na mbili hivyo watatakiwa kuzilipa,” alisema Mwaluka.

 

Wakati huohuo, Mwaluka amesema tayari ametengeneza mlango huo sababu bado kulikuwa na mchezo wa mwisho wa ligi kati ya Mbeya City dhidi ya Biashara United jana Jumapili.

 

DERICK LWASYE, Mbeya

The post Gwambina Yavunja Mlango, Yadaiwa Laki Tano appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz