Fei Toto: Wanayanga Kuna ‘Sapraizi’ Yenu Kigoma-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Fei Toto: Wanayanga Kuna ‘Sapraizi’ Yenu Kigoma-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji fundi wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum ‘FeiToto’, amefunguka kuwa baada ya kukamilisha michezo yao ya Ligi Kuu Bara, sasa wanajipanga vizuri na mchezo wa fainali ya shirikisho dhidi Simba utakaopigwa Julai 25, mkoani Kigoma huku akiahidi kuwa kuna Sapraizi wamewaandalia Wanayanga.

 

Vigogo hao wa soka la Tanzania watakutana kwenye mchezo wa fainali hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

Yanga wataingia katika mchezo huu na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kwenye mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Julai 3, mwaka huu.

 

Fei Toto amekuwa kwenye fomu ya hali ya juu chini ya kocha Nasreddine Nabi, ambapo mpaka sasa msimu huu nyota huyo amefanikiwa kufunga mabao matano.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Fei Toto alisema: “Kiukweli kila mchezaji ndani ya kikosi chetu ana ari kubwa kuelekea mchezo wetu wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, bila shaka utakuwa mchezo mgumu kwa sababu ni fainali na kila timu ina malengo ya kushinda kombe hilo.

 

“Lakini niwaahidi Wanayanga kuwa kuna kitu cha tofauti wanakwenda kukipata kwenye mchezo huo, hivyo wasikose kujitokeza kutusapoti kwa wingi.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Fei Toto: Wanayanga Kuna ‘Sapraizi’ Yenu Kigoma appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz