ARGENTINA YATINGA FAINALI COPA AMERICA KWA MATUTA, KUKUTANA NA BRAZIL JUMAPILI-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

ARGENTINA YATINGA FAINALI COPA AMERICA KWA MATUTA, KUKUTANA NA BRAZIL JUMAPILI-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
ARGENTINA imetinga fainali ya Copa America kwa ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 na Colombia ndani ya dakika 120 Alfajiri ya leo Uwanja wa Brasília.
Shujaa wa Argentina alikuwa ni kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez, aliyeokoa penalti tatu za Colombia.
Mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martínez alianza kuifungia Argentina dakika ya saba akimalizia pasi ya Nahodha, Lionel Messi, kabla ya mshambuliaji wa Porto, Luis Díaz kuisawazishia Colombia dakika ya 61 akimalizia pasi ya Edwin Cardona.


Na kwenye mikwaju ya penalti, Messi, Leandro Paredes na Lautaro Martínez waliifungia Argentina huku Rodrigo De Paul pekee akikosa na kwa Colombia waliofunga ni Juan Cuadrado na Miguel Borja pekee walifunga huku Davinson Sánchez, Yerry Fernando Mina na Cardona wakikosa.
Sasa Argentina itakutana na wenyeji, Brazil katika fainali ya Copa America Jumapili Uwanja wa Jornalista Mário Filho, au Maracanã Jijini Rio de Janeiro, wakati Colombia itawania nafasi ya tatu dhidi ya Peru Jumamosi.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz