YANGA SC YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA U20 BAADA YA KUICHAPA MWADUI FC 3-0 CHAMAZI -Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

YANGA SC YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA U20 BAADA YA KUICHAPA MWADUI FC 3-0 CHAMAZI -Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
 TIMU ya Yanga imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa Kundi A, mabao ya Yanga B inayofundishwa na Said Maulid 'SMG' yamefungwa na Abby Mikimba dakika ya 12 na Abdulkarim Yunus mawili, dakika ya 44 na 48.
Yanga SC imemaliza mechi tatu za Kundi A na pointi saba, ikishinda mbili, nyingine 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na sare ya bila kufungana na watani wao wa jadi, Simba.
Maana yake wanatinga Nusu Fainali ya michuano hiyo.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz