Shilole Kumburuza Nuh Mziwanda Kortini - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Shilole Kumburuza Nuh Mziwanda Kortini
KIKI anayotumia Msanii wa Bongofleva, Nurdin Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwa kumhusisha msanii mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ katika kupaisha muziki wake sasa imemtokea puani.

 

Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni ametoa ngoma inayokwenda kwa jina la Saudia, amedaiwa kumtumia Shilole katika kuipa promo ngoma hiyo ambayo hadi juzi ilikuwa na watazamaji zaidi ya 11,000 katika mtandao wa Youtube.

 

Hata hivyo, kabla ya kuachia ngoma hiyo, Nuh aliposti picha iliyomuonesha Shilole akiwa amejichora tattoo yenye jina la Nuh katikati ya kifua chake.

 Kama hiyo haitoshi, Nuh aliposti video iliyomuonesha akielezea hisia zake dhidi ya Shilole huku akimuomba warudiane.Nuh aliendelea kumuandama Shilole ambaye hivi karibuni amefunga ndoa na Rajab Issa ‘Rommy’ bila kujali kuwa anaweza kuvunja ndoa hiyo.

 

SHILOLE AMUONYA

Kufuatia drama hizo za Nuh, Shilole alimtaka msanii huyo kumheshimu kwa sababu sasa yupo kwenye ndoa inayotambulika kisheria.

 

Akizungumza na kituo kimoja cha runinga Shilole alisema “Naomba sana asinifuatilie maisha yangu aniheshimu kwa sababu mimi ni mke wa mtu, tena tumefunga ndoa kabisa inayotambulika.

 

”Hata hivyo, licha ya onyo hilo, Nuh aliendelea kuposti picha na video za zamani kipindi walipokuwa kwenye mapenzi motomoto, jambo linalotajwa kuwa linalenga kumdhalilisha Shilole. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Shilole, amelieleza RISASI Jumatano kuwa tayari Shilole ameliripoti tukio hilo katika kituo kimoja cha polisi kwa lengo la kumburuza Nuh mahakamani.


Licha ya kwamba awali Nuh alipohojiwa na kituo hicho cha runinga alidai kuwa alikuwa anamtania Shilole, lakini juzi aliposti ujumbe mfupi wa maneno akieleza kuwa ameitwa katika kituo cha polisi.Aliandika, “Nimepata simu kutoka Oysterbay polisi… naheshimu sana nitakuja hapo”.

Ujumbe huo wa Nuh ulidhihirisha kuwa tayari Shilole ameanza kumchukulia hatua za kisheria kutokana na matukio ya udhalilishaji anayodaiwa kuendelea kumfanyia katika mitandao ya kijamii.
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz