RONALDO APIGA MBILI URENO YAICHAPA HUNGARY 3-0 -Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

RONALDO APIGA MBILI URENO YAICHAPA HUNGARY 3-0 -Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
URENO imeanza vyema Euro 2020 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Hungary katika mchezo wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest.
Mabao ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Raphaël Guerreiro dakika ya 84 na Nahodha Cristiano Ronaldo dakika ya 87 ka penalti na 90 na ushei akimalizia pasi ya Rafa Silva.
Ronaldo anakuwa mfungaji wa mabao mengi kihistoria kwenye fainali za Kombe hilo la Mataifa ya Ulaya, 11 akimpiku Mfaransa Michel Platini.Wakati Platini alifunga mabao yake yote kwenye fainali za mwaka 1984 pekee, Ronaldo amefunga kwenye fainali tano tofauti.
Mechi nyingine ya kundi hilo, Ufafansa imewafunga wenyeji,  Ujerumani 1-0, bao la kujifunga la beki Mats Hummels dakika ya 20 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz