POLAND YAANZA VIBAYA EURO 2020, YAPIGWA 2-1 NA SLOVAKIA-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

POLAND YAANZA VIBAYA EURO 2020, YAPIGWA 2-1 NA SLOVAKIA-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
TIMU ya taifa ya Poland imeanza vibaya Euro 2020 baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Slovakia katika mchezo wa Kundi E usiku wa jana Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg, Urusi.
Kipa Wojciech Szczęsny wa Juventus alijifunga dakika ya 18 kuipatia Slovakia bao la kwanza, kabla ya beki wa Inter Milan Milan Skriniar kufunga la pili dakika ya 69, wakati bao la Poland lilifungwa na kiungo wa Torino Karol Linetty dakika ya 46.
Nayo Scotland ilichapwa 2-0 na Jamhuri ya Czech Republic, mabao ya mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Patrik Schick dakika ya 42 na 52 katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Venue Hampden Park Jijini Glasgow.


Hispania ikalazimishwa sare ya bila kufungana na Sweden katika mchezo mwingine wa Kundi E Uwanja wa Olimpico de Sevilla Jijini Sevilla.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz