Mkude, Kagere Waongeza Miaka Miwili Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mkude, Kagere Waongeza Miaka Miwili Simba-Michezoni leo

WAKATI ikielezwa kwamba Yanga inawavizia Meddie Kagere na Jonas Mkude waachwe na Simba ili wawasajili, habari mbaya kwao ni kwamba, nyota hao kila mmoja akiongeza mkataba wa miaka miwili.

 

Mbali na nyota hao, pia kipa aliyekosa nafasi kubwa ya kucheza kikosini hapo, Beno Kakolanya, naye ameongeza miaka mingine miwili kuendelea kuwa ndani ya Simba.

 

Nyota hao walikuwepo sehemu ya wachezaji ambao mikataba yao ilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini kutokana na umuhimu wao, wameongezewa.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, tangu miezi miwili iliyopita, Simba imemalizana na Mkude na Kagere baada ya kuwasainisha kwa siri.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, mabosi wa Simba wamewasainisha nyota hao mikataba baada ya kupata taarifa za kuwindwa na Yanga.“Tulikuwa tunawaangalia Yanga wakiendelea kupiga kelele za kuhitaji saini za wachezaji wetu Kagere na Mkude, nikuhakikishie kuwa, wachezaji hao walisaini mikataba miezi miwili iliyopita.

 

“Kama Simba ingekuwa haijamuongezea mkataba Mkude isingepata tabu ya kuhangaika naye mara kumpeleka hospitali kumpima na badala yake tungeachana naye. Ukweli ni kwamba Mkude na Kagere bado wataendelea kuichezea Simba hadi 2024.

“Kakolanya yeye alisaini mkataba Jumatatu usiku, ni baada ya benchi la ufundi kupendekeza aongezewe mkataba wa miaka miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Simba kupitia kocha wake mkuu, Mfaransa, Didier Gomes, hivi karibuni alisema: “Wachezaji wote nitakaowahitaji hawataondoka Simba na badala yake nitawaongezea mikataba.

 

“Ninafurahia kufanya kazi na wachezaji wangu muhimu ambao wameipambania timu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo nisingetamani kuona wanaondoka na badala yake waendele kubakia hapa.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, DAR

The post Mkude, Kagere Waongeza Miaka Miwili Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz