Mastaa Wawili Waivuruga Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mastaa Wawili Waivuruga Simba-Michezoni leo

Mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Perfect mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Perfect Chikwende.

KLABU ya Simba, inafikiria kusitisha mkataba wa kiungo wake mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Perfect Chikwende huku ikipanga kumuongezea mkataba Francis Kahata.

 

Mkataba wa Kahata unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

 

Simba ilimsajili Chikwende katika usajili wa dirisha dogo msimu huu maalum kwa ajili ya Ligi Kuu Bara, akichukua nafasi ya Kahata ambaye yeye aliwekwa maalum katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Simba inafikiria kuachana na Chikwende baada ya kushindwa kuonyesha ushindani katika kikosi cha Mfaransa, Didier Gomes.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mshambuliaji huyo amepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi, pia kukaa benchi la wachezaji wa akiba.

 

Aliongeza kuwa, uongozi huo hivi sasa unafikiria kumuongezea mkataba Kahata ikiwezekana arejeshwe katika kikosi cha wachezaji watakaocheza ligi kuu na mashindano mengine msimu ujao akichukua nafasi ya Chikwende.

 

“Kilichotokea kwa Chikwende kila kiongozi akitegemei ni baada ya kushindwa kuonesha kile ambacho walichokuwa wanakihitaji baada ya kutua Simba.“Hivyo uongozi unafikiria jinsi ya kuachana naye, lakini wanapata ugumu wa kusitisha mkataba wake kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho watatakiwa kumlipa kutokana na muda wa mkataba ambao ameusaini.

 

Upo uwezekano mkubwa wa Simba kumuongezea mkataba Kahata, kwani yeye tayari alikuwa amezoea mazingira ya ligi hapa nyumbani tofauti na Chikwende ambaye amefeli,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Mkuu wa Mahudhui wa Simba, Ally Shatry kuzungumzia hilo, alisema: “Masuala yote ya usajili hivi sasa yapo chini ya Bodi ya Wakurugenzi wa Simba na siyo kwangu.

 

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, hivi karibuni alizungumzia usajili na kusema: “Suala la usajili hivi sasa tumeliachia benchi la ufundi ndiyo ambalo linajua mchezaji gani wa kusajiliwa na kuachwa, sisi viongozi kazi yetu utekelezaji tu.”

The post Mastaa Wawili Waivuruga Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz