Makambo, Yanga Kimeeleweka-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Makambo, Yanga Kimeeleweka-Michezoni leo

SASA rasmi mshambuliaji kipenzi cha Yanga, Mkongomani, Heritier Makambo anatua Jangwani baada ya kufikia muafaka mzuri.

 

Makambo ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye mipango ya kusajiliwa na Yanga tangu msimu uliopita kabla ya dili lake kutokamilika na kuendelea kubaki kuichezea Horoya AC ya Guinea. Mshambuliaji huyo aliitumikia Yanga msimu wa 2018/19.

 

Kuelekea msimu ujao, Yanga imepanga kukifanyia maboresho kikosi chake ikiwemo kufanya usajili kwenye safu ya ushambuliaji, kiungo na beki.Kwa mujibu wa taarifa ambazo Spoti Xtra, Yanga imefikia makubaliano hayo mazuri baada ya mshambuliaji huyo kuonesha nia ya kujiunga na timu hiyo.

 

Mtoa taarifa huyo alisema, Yanga tayari imefanya mawasiliano na viongozi wa Horoya ambao wenyewe wamekubali kumuachia mshambuliaji huyo aliyebakisha msimu mmoja kwenye mkataba wake wa kukipiga hapo.Aliongeza kuwa, Yanga itaingia kwenye gharama ya kununua mkataba wa mwaka mmoja alioubakisha Horoya kama ilivyokuwa kwa Wakongomani, Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda walipojiunga na Yanga msimu huu.

 

“Makambo ni uhakika anarudi Yanga msimu ujao, ni baada ya yeye kuonesha nia, hivyo suala lipo kwa viongozi wa Yanga ndiyo wenye kibarua cha kuusitisha mkataba wake wa msimu mmoja uliobaki huko alipo.“Hivi sasa kila kitu kinakwenda vizuri katika usajili wake, ni baada ya Yanga wenyewe kuwafuata Horoya ambao wameonekana kukubali kumuachia mshambuliaji huyo.

 

Uzuri Makambo mwenyewe ndiye ameonesha nia ya kuja Yanga, atakuja na straika mwingine wa kimataifa,” alisema mtoa taarifa huyo.Mtu wa karibu wa Makambo, amefichua ujumbe aliotumiwa na straika huyo uliosomeka: “Nimeimisi Yanga, Nimemisi Tanzania.

 

Yanga kupitia Kocha Mkuu raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, alisema: “Nimepanga kukifanyia maboresho kikosi changu katika msimu ujao kwa kusajili wachezaji wenye uwezo watakaoisaidia timu kimataifa.”Yanga hadi hivi sasa imekamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao ni kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu na beki wa KMC, David Bryson.

WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

The post Makambo, Yanga Kimeeleweka appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz