HALMASHAURI YA GEITA KUJENGA UWANJA WA MICHEZO KWA GHARAMA YA SH. BILIONI 1.9 UTUMIKE KWENYE LIGI KUU-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

HALMASHAURI YA GEITA KUJENGA UWANJA WA MICHEZO KWA GHARAMA YA SH. BILIONI 1.9 UTUMIKE KWENYE LIGI KUU-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

Na Alphonce Kabilondo, GEITA

HALMASHAURI ya Mji wa Geita Mkoani Geita imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya kujenga Uwanja mpya wa mpira utakaotumika katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara utakaokuwa na uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 18,000.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhandisi Felix Nlalio ametoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo mbele ya kamati ya siasa ya wilaya ya Geita ilipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo .
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa mchakatao wa kumpata mkandarasi wa kujenga uwanja huo umeshamilika na kwamba halmashauri imetenga fedha hiyo ambayo ni mapato ya ndani pamoja na shilingi bilioni moja ambayo ni fedha ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii CSR kutoka Mgodi waa GGML.


Alisema kuwa wakati ujenzi wa uzio ukiendelea utaenda sanjari na usanifu wa majukwaa na kupanda nyasi za (ukoka) na baadae zitawekwa nyasi za bandia ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa kipindi cha miezi minne .
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita Mkoani Geita , Barnabas Mapande alisema kuwa  mbali na wananchi kupata nafasi kushudia burudani ya soka kufuatia mitanange ya timu za lingi kuu  itakayokuwa ikiendeea katika uwanja huo pindi utakapo kamilika halmashuri pia itakusanya mapato.
 ''Uwanja huu ni muhimu kwa wanageita kwa kuwa sasa tunayo timu ya Geita Gold Fc ambayo imefuzu kushiriki michezo ya ligi kuu hivyo uwanja ukamilike haraka ''alisema mwenyekiti huyo .
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwalimu Fadhili  Juma alisema kuwa kiu kubwa ya wanageita ni kushudia ligi kuu inachezwa  kwenye dimba la Geita.
Mkuu huyo alisema kuwa hivikaribuni Rais wa shirikisho la soka Nchini TFF Wallace Karia  alifika Geita na kutembelea eneo la Magogo kata ya Bombambili  unapojengwa uwanja huo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuleta watalaamu waliobobea kusanifu viwanja vya soka.


Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz