Bocco Apewa Tuzo ya Kagere Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bocco Apewa Tuzo ya Kagere Simba-Michezoni leo

KASI ya kufunga mabao aliyonayo mshambuliaji na nahodha wa kikosi cha Simba, John Bocco imemuibua kocha wake Mtunisia, Adel Zrane ambaye amesema ana imani kubwa mshambuliaji huyo ndiye atakayeibuka na tuzo ya ufungaji bora msimu huu.

 

Bocco ambaye Jumapili iliyopita alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata Taifa Stars kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi, amekuwa na wakati mzuri ndani ya kikosi cha Simba ambapo mpaka sasa ameifungia mabao 13 yanayomuweka katika nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora msimu huu nyuma ya Prince Dube wa Azam mwenye mabao 14.

 

Mshambuliaji huyo amefunga mabao saba katika michezo minne mfululizo iliyopita ya michuano mbalimbali, aliyoshuka uwanjani kuichezea Simba na timu ya Taifa Stars.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha Zrane alisema: “Vita ya ufungaji bora msimu huu inaonekana kuwa na ushindani mkubwa sana, misimu miwili iliyopita mshambuliaji wetu, Meddie Kagere alitwaa tuzo hiyo mfululizo, lakini msimu huu tayari Dube wa Azam, na Bocco wameongezeka kwenye huo ushindani.

 

“Lakini licha ya kasi aliyonayo Dube mwenye mabao 14, nakuhakikishia kuwa mfungaji bora wa msimu huu atakuwa Bocco kwa kuwa ana kila sababu ya kufanya hivyo, zaidi ya hiyo nina uhakika kuwa Dube atamaliza katika nafasi ya tatu kwani mfungaji bora namba moja na yule wa pili wa ligi watatoka ndani ya kikosi cha Simba.”

STORI: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Bocco Apewa Tuzo ya Kagere Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz